Zaka ya madeni
Deni
Mali ambayo ni lazima kulipwa na mtu aliyechukua mkopo.
Hukumu ya zaka ya madeni yanayowajibika kulipwa na mtoaji zaka.
Ikiwa mtu ana deni kiwango chake chafika nisabu au kiko chini ya nisabu basi deni hili halimuwajibishi mtu huyu kutoa zaka. Na ikiwa deni halipunguzi nisabu basi atatowa kutoka kwa mali yake kiwango cha deni hilo, na atowe zaka katika mali iliyobaki.
Mfano: Ikiwa mtu ana (Dolari 10000), na deni (anadaiwa) (Dolari 10000), basi haimlazimu kutoa zaka; kwasababu deni hilo limemaliza nisabu, na vile vile ikiwa deni ni (Dolari 9950), basi deni hili linapunguza nisabu hivyo basi hawajibiki kutoa zaka, ama ikiwa deni lake ni (Dolari 4000), basi atapunguza kutoka kwa mali yake kiwango cha deni hilo, na itabakia na (Dolari 6000) ambazo zinawajibika kutolewa zaka
Isipokua achukue mtu deni na asitumie kwa lengo la kibiashara, kama mtu anunue nyumba kwa njia ya kulipa kidogo kidogo (hire purchase)au atumie deni kwa kufanya miradi ambayo inaokadiriwa kwa mamilioni ya pesa, huenda akaamua mmoja wa wafanyi biashara kupanua biashara yake, na kunua kutoka kwa pesa hizo jambo la kuzalisha, je deni hilo lilo zalisha mali itaangusha zakaa?
Kusema hizo ni kupotea mali inaopaswa kutoa zakaa kwa mafukara, pia inamaana kua wafanyi biashara wa leo hawaruhusiwi kutoa zakaana limemelizika kungamao lilofanywa kuweit mwaka wa 1409 hijri sawa na 1989 Miladi kwa yanayofuata: